Sambaza....

Mechi ya pili ya Simba kwenye uwanja wa ugenini. Ndanda FC walikataa uteja kwa Simba!. Mechi nane (8) kabla ya mechi ya msimu huu dhidi ya Ndanda FC , Simba walikuwa wameshinda mechi zote nane. Ndanda FC msimu huu amejifariji kidogo kwa suluhu ya bila kufungana.

Simba anaenda CCM Kirumba , eneo ambalo ni ngumu kwake. Simba na Mbao katika uwanja wa CCM Kirumba wamekutana mara mbili ambapo Simba ameshinda mechi moja na kutoka sare moja.

Kwanini mechi hii ni mechi yenye mabao mengi?

Katika mechi mbili zilizochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba imezalisha mabao tisa (9) ambapo Simba imefunga magoli matano (5) na Mbao imefunga magoli manne (4).

Mbao ana nafasi ya kushinda mechi hii??

Mechi dhidi ya Simba ni tofauti na mechi ya aina dhidi ya timu za kawaida.

Mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mbao ilifungwa goli moja.

Hivo mechi dhidi ya Simba itakuwa na maandalizi tofauti na mechi iliyopita kuanzia nje ya uwanja mpaka ndani ya uwanja , utofauti ambao utaleta ushindani mkubwa ndani ya uwanja.

Ushindani huu utaleta ugumu kwenye mechi hii?

Hapana shaka utaleta ushindani kweñye mechi hii. Kwanini?, Simba wametoka kupata suluhu dhidi ya Ndanda FC. Suluhu ambayo inaweza kuonekana katika mionekano miwili kwenye mechi hii.

Muonekano wa kwanza, ni huu. Kama Simba watachukulia matokeo yaliyopita katika hali hasi na Mbao wakayachukulia matokeo ya Mbao na Simba katika hali chanya mechi hii itakuwa ngumu kwa Simba , kwa sababu Simba watakuwa na Ombwe la mechi iliyopita na Mbao watapata nguvu kuwa Simba kwenye mechi ya ugenini msimu huu kapoteza alama 2.

Ukuta wa Simba unaweza kuwa sehemu ambayo inaweza kuamua mchezo wa Leo?

Ukitizama kuanzia katika mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Mtibwa Sugar mpaka mechi iliyopita dhidi ya Ndanda FC , Simba imefungwa goli moja tu katika mechi nne. Hivo ukuta huu wa Simba unaweza ukawa kikwazo kwa Mbao kama wakitanguliwa kufungwa.

MWISHO.

Mechi ya mwisho kwa Simba kwenye uwanja wa CCM Kirumba ilishinda dhidi ya Mtibwa Sugar, tangu ishinde Simba imekuwa ikipitia kipindi ambacho mashabiki wengi wa Simba wamekuwa hawaridhiki na kiwango chake, tunaweza tukasema Simba inapitia kipindi ambacho watu wengi hawaridhiki na kiwango chake, hii inaweza kuharibu hali ya kujiamini kwa wachezaji kama hawatatengezwa vizuri.

Mbao wanatakiwa kufikiria makosa ambayo waliyafanya katika mechi dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wao wa nyumbani ili kufanya vizuri katika mechi ya leo. Matokeo yaliyopita yatumike katika kuwajenga katika mechi ya leo na siyo kuwabomoa.

Sambaza....