Sambaza....

KATIKA michezo rasmi nane iliyopita Yanga SC imeruhusu jumla ya magoli 17 -wastani wa magoli mawili katika kila mchezo. Na magoli mengine matatu katika michuano ya SportPesa. Ni mchezo mmoja tu hawakuruhusu goli lolote. Hii inamaanisha timu hiyo inapaswa kujitazama na kujisahihisha katika ulinzi.

Jukumu la ulinzi uwanjani ni kwa kila mchezaji, lakini mabeki na golikipa wanatakiwa kuwa makini zaidi kwasababu hili jukumu linalowafanya wawepo uwanjani, hata kama viungo na washambuliaji pia watafanya hivyo.

Image result for kindoki yanga

Yanga inawezekana haina kipa wa kiwango cha juu kwa miezi 15 sasa, lakini ukitoa makosa ya Mcameroon, Youthe Rostand, Beno Kakolanya na Mcongoman, Klaus Kindoki safu yao ya ulinzi wa kati ina-nyufa kubwa.

Vicent Andrew alihusika katika goli la kuongoza la Stand United katika mchezo wa jana Jumapili na muda wote aliocheza na nahodha Kelvin Yondan kama walinzi-pacha hawakuonekana kuelewana.

Walijichanganya mara nyingi na hakuna kati yao aliyeonekana kucheza vizuri kama beki wa mwisho na hili linawakumbusha mapema kuwa wanapaswa kusajili beki bora mwenye uzoefu wakati wa dirisha dogo mwezi Disemba.

Katika michezo sita ya Caf Confederations Cup Rostand aliruhusu magoli 11 na Beno magoli mawili. Jumla magoli 13. Katika michezo miwili ya ligi kuu msimu huu- Beno ameruhusu goli moja na Klaus magoli matatu, jumla magoli manne- ukijumlisha na yale 13 ya Caf utaona jumla ya magoli 17 wamefungwa makipa watatu tofauti chini ya ulinzi ule ule, lakini makocha tofauti.


: USM Alger 4-0 Yanga- CCC
: Yanga 0-0 Rayon Sports Club- CCC
: Kakamega Homeboyz 3-1 Yanga- SportPesa Super Cupp: Gor Mahia FC 4-0 Yanga – CCC
: Yanga 2-3 Gor Mahia- CCC
: Yanga 2-1 USM- CCC
: Rayon 1-0 Yanga – CCC
: Yanga 2-1 Mtibwa Sugar FC – TPL
: Yanga 4-3 Stand United- TPL


Kwa matokeo kama haya haipaswi kumlaumu golikipa pekee bali ni kila mmoja kujitazama na kujisahihisha katika makosa yao. Tulimlaumu Youthe kwa makosa yake ya mara kwa mara, ma kama bebi haitarekebisha makosa yao Klaus na Beno pia tutawasema lakini tatizo linaanzia kwa Kelvin na Andrew.

Sambaza....