Hapana shaka siyo mara yako ya kwanza kuona hili neno kwenye makala zangu “kila kitu kwenye dunia hii ya sasa ni biashara”.
Ndicho kitu ambacho mimi nakiamini kwa sababu tuko kwenye dunia ya aina hii. Dunia ambayo watu wengi hufikiria kufanya chochote ili wapate faida.
Faida ambayo huja baada ya uwekezaji wa akili za kibiashara kwenye jambo husika.
Leo hii tunaamini mpira wetu ni wa kulipwa, kitu ambacho kipo kwenye karatasi tu na hakipo kwenye uhalisia.
Huwezi kusema mpira wetu ni wa kulipwa ilihali hakuna mazingira mazuri ya kibiashara kwenye mpira wetu.
Viwanja vinavyotumika kwenye ligi kuu havina miundo mbinu ya kibiashara, ni viwanja ambavyo havitoi nafasi kwa kumwaminisha mtu kuwa mpira ni sehemu ya mtoko.
Waamuzi wamekuwa wakiua dhana ya kibiashara kwenye mpira kwa sababu wanatupa matokeo ambayo siyo haki ndiyo maana hata mauzo ya tiketi huwa ni haba kwa sababu ya vitu kama hivi vinavyovunja mioyo ya watu wengi.
Leo hii kulikuwa na mkutano wa waandishi wa habari na shirikisho la mpira Tanzania (TFF). Mkutano ambao mara nyingi hubeba sura ya shirikisho la soka Tanzania (TFF). Ni mkutano ambao kibiashara unatumika kama sehemu ya kukuza mahusiano ya jamii “Public Relation” (PR).
Sehemu kubwa ya PR ni visibility. (Visual, yani vitu vinavyoonekana, mfano labda sehemu unayofanyia press inaonekanaje?, Yani PR kwa kiswahili cha mjini ni “KIKI”. Yani unafanya kitu kinachoonekana ili kikubebe kwenye biashara yako.
Mfano, kutengeneza mazingira mazuri ya kufanyia Press hii ni ” KIKI” ya kuibeba biashara yako. Watu watakuona wewe ni smart, na watakuja kwako kuwekeza pesa kwa sababu your smart.
Mazingira ambayo unachagua kufanyia mkutano na waandishi ya habari ndiyo mazingira ambayo yanakuelezea wewe.
Yani wewe ni mtu wa aina gani?, Ndiyo mazingira ambayo yanaweza kumvutia mfanyabiashara yeyote yule ili aje awekeze pesa zake kwa sababu ya muonekano wako wa nje.
Mpangilio mzuri wa sehemu unayofanyia mkutano na waandishi wa habari ni “KIKI” Inayoweza kukuuza sana. Inawezekana katika mkutano wa Leo na waandishi wa habari , TFF walijua kuwa ni kikao cha kamati ya harusi ndiyo maana hawakujali mazingira ambayo waliyafanyia.
Mazingira ambayo hata viti wakivyokalia vilikuwa vitu vya kampuni moja ya vinywaji baridi. Kampuni ambalo halina ubia na TFF. TFF waliamua kukaa tu ili mradi wake na waongee tu bila kujali kitu chochote.
Hapa ndipo linapokuja kukubaliana na maneno ambayo nafsi yangu huwa inaniambia kila siku kuwa TFF siyo nembo kubwa “brand” bali ni shirikisho maarufu “popular association”.
Brand ni kitu kingine kikubwa sana kukiandika kwenye sentensi moja. Brands inakuwa na demage sana ikichafuliwa. TFF ni popular association ila TFF haijajengwa kama brand association. Mpaka sasa TFF is not a brand , its popular association. Ndiyo maana wanafanya vitu vya kawaida kwenye hali isiyo ya kawaida.
Hawajipi thamani wao kama wao, hawaoni umuhimu mkubwa wa kutangaza bidhaa fulani ambayo hawana ubia nao kwa kukalia viti vyenye nembo vya bidhaa hiyo. Kwao wao ni kawaida kwa sababu wanafanya kama shirikisho maarufu na siyo kama shirikisho lenye nembo ya kibiashara.
Hata chumba walichochagulia kufanya mkutano na waandishi wa habari kilichaguliwa ili mradi tu watu waongee waandishi wapate cha kuhabarisha wananchi. Hawakufikiria hasara za kibiashara kufanyia mkutano na waandishi wa habari kwenye chumba kile.
Na hii ni moja ya sababu kwanini ligi yetu haina mdhamini kwa sababu shirikisho letu hatulithamini na bidhaa zake hatuzithamini. Ni ngumu kwa mfanyabiashara kuweka pesa sehemu ambayo watu wake hawajithamini