Raundi ya Tatu mzunguko wa kwanza wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Ijumaa kwa mchezo mmoja ambapo katika dimba la Namfua mkoani Singida kutakuwa na patashika Nguo kuchanika.
Baada ya kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu Tanzania bara, ‘Wabishi’ Kikosi cha Mbao FC Wababe wa vigogo hii leo wataumana na wakamua Alizeti Singida united pale mkoani Singida.
Mchezo huo wa tatu kwa timu zote utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Singida united uwanja wa Namfua.
Mbao ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu Bara inakumbukumbu nzuri katika michezo yake baada ya kuichapa Alliance 1-0 mechi ya kwanza kabla ya kufanikiwa kushinda 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga na kuondoka na pointi tatu.
Singida united wenyewe Kabla ya mchezo huu walifungwa mechi ya kwanza goli 1-0 na Biashara united kabla ya kushinda mechi yao ya pili dhidi ya mwadui goli 1-0 .
Ratiba TPL kesho.