Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba hayumo kunako kikosi cha Yanga sc, kilichoondoka leo kuelekea Hawassa, nchini Ethiopia tayari kwa mchezo wa marejeano wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho dhidi ya Wolaita dicha
Kikosi cha wachezaji 20, na viongozi 12, kimepanda ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia kwenda Addis Ababa na baadae kuunganisha kwa basi kwenda katika mji wa Hawassa utakapopigwa mchezo huo
Wachezaji waliosafiri hii leo ni magolikipa Youth Rostand, Beno Kakolanya
Walinzi Hassan Kessy, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Gardiel Michael, Abdallah Shaibu, Kelvin Yondan na nahodha Nadir Haroub Ally Upapa
Viungo ni Pappy Tshitshimbi, Yusuf Mhiru, Pius Buswita, Raphael Daud, Said Juma “Makapu”, Juma Mahadhi, Geoffrey Mwashiuya, Emmanuel Martin na Thaban Kamusoko
Washambuliaji ni Obrey Chirwa na Yohana Mkomola
Yanga sc, watakuwa wageni wa Wolaita dicha Jumatano jioni kunako dimba la Hawassa City huku ikiwa na mtaji wa mabao 2-0 iliopata nyumbani kunako uwanja wa taifa Jumamosi iliyopita
Katika mchezo huo wa marejeano ambao Yanga sc, wanatakiwa kucheza kufa na kupona kulinda ushindi wao, hawatakuwa na kocha wao mkuu Mzambia George Lwandamina aliyetimka kunako klabu hiyo na kurejea Zesco ya nchini mwao
Hivyo Yanga sc itakuwa chini ya waliokuwa wasaidizi wa Lwandamina Mzambia mwenzake Noel Mwandila na wazawa Shadrack Nsajigwa, Juma Pondamali