Mchezo wa soka kati ya Singida United dhidi ya Yanga sc umemalizika kwa Singida kupata ushindi wa penati 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za Mchezo.
TATHIMINI!
Nikianza na wenyeji Singida United ambao waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-4-2 flat.
Hakika Singida United walikuwa bora sana kimbinu na kiufundi, silaha yao ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha wanamiliki mpira kitu ambacho kwa kiasi fulani naweza sema walifanikiwa kwa vipindi vyote. Waliweza kutoka kwa counter attacking play ama short pass style na mara nyingi walikifumua kiungo cha Yanga kwa muunganiko huo mzuri, huku kiungo Tafadhza Kutinyu akiwa mwiba kwa wachezaji wa Yanga. Hivyoo kupelekea kupata bao la kusawazisha kupitia Kenny Ally, baada ya gonga safi za viungo wa Singida utd.
Kiujumla Singida walistahili ushindi, authority yao ya mchezo ilikuwa nzuri sana kulinganisha Yanga, kwenye tactical philosophy, tactical focus, team technical understand, changing position na style of play Singida walikuwa bora.
Yanga sc, waliingia kwenye mchezo huo wakitumia mfumo wa 4-4-2 huku kwenye eneo la kiungo likionekana kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu, Said Juma alicheza kama kiungo wa ulinzi mara nyingi alishindwa kutoa back-up ama kuwatawanya viungo wa Singida ili kumfanya Papy Tshishimbi kuwa kiungo huru wa kuchezesha timu. Kwa kiasi kikubwa hii ndio sehemu ya ambayo ilichangia kwa Yanga kuzidiwa na Singida utd.
Sehemu ya pili ni kukosa ubunifu kwenye eneo la ushambuliaji, mara nyingi walijaribu kwenda kwenye attacking adminstration kwa kutumia high balls, aina hii ya mipira haikuwa na faida kwao hasa kutokana na kukosa mshambuliaji sahihi wa kupokea aina hii ya mipira, hali iliyopelekea kushindwa kumiliki mpira na kujikuta muda mwingi wanacheza mchezo wa kujilinda zaidi.
Attacking tactics, pressing game, counter attacking run, flow fluid ama direct play hawakuwa vizuri sana.
NB: Mazingira ya uwanja kwa kiasi fulani yalichangia kupunguza ladha ya mchezo. Mvua kubwa iliyonyesha muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo na pia wakati mchezo ukiendelea iliuathiri , kwa maana baadhi ya maeneo kulikuwa na maji hali ilipelekea mipira mingi kukwama kutokana na uwanja kua na madimbwi ya maji.
Na. Jemedari Abdallah
0654 359469