Sambaza....

Chama cha soka cha visiwani Zanzibar (ZFA) kimemsimamisha mwamuzi wake,Mfaume Ally Nassor, kwa muda ili kupisha uchunguzi dhidi yake kwa tuhuma za kupanga matokeo

Mwamuzi huyo kutoka visiwani humo, pamoja na waamuzi wengine Frank Komba, Israel Mujuni Nkongo na Soud Lila kutoka Tanzania bara wanachunguza na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa tuhuma za upangaji matokeo

Waamuzi hao kutoka Tanzania walichezesha mchezo wa ligi ya vilabu bingwa Afrika kati ya Lydia Ludic ya Burundi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, mchezo uliopigwa Februali 21, 2018 mjini Bujumbura

Taarifa zinaeleza kuwa kabla ya mchezo huo, viongozi wa Rayon walifika kunako hotel waliyofikia waamuzi hao huku ushahidi wa picha Cctv ukimuonesha Ofsa mmoja wa Rayon akiingia kunako chumba walimo kina Mfaume

Shirikisho la soka Tanzania TFF bado halijatoa tamko kuhusu waamuzi wake wanaochunguzwa, huku likithibitisha kupokea taarifa hiyo na kusema wanaacha uchunguzi ufanyike

Sambaza....