Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga sc, leo hii imefanikiwa kusonga mbele kunako michuano ya ligi ya vilabu bingwa barani Afrika, baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na wenyeji St Louis ya Shelisheli

Mchezo huo wa mzunguko wa awali wa marejeano ulipigwa kunako dimba la Linite mjini Victoria nchini Shelisheli

Kwa matokeo hayo yanaifanya Yanga sc, kusonga mbele kwa matokeo ya jumla ya 2-1 mara baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Tanzania

Katika mchezo wa leo, hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga sc walikuwa mbele kwa bao moja likifungwa na kiungo wake wa ushambuliaji Ibrahim Ajib kunako dakika ya 43, aliyemalizia kazi nzuri ya mlinzi Hassan Kessy

Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwaamsha St Louis, na kuanza kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa Yanga lakini walinzi wake wakiongozwa na nahodha Nadir Haroub “Canavaro walikuwa imara kuzima mashambulizi hayo

Kipindi cha pili Yanga sc walionekana kucheza zaidi kimbinu kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza ili kutafuta bao la pili lakini washambuliaji wake walikosa utulivu na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga

Na zikiwa zimethalia dakika nne mchezo kumalizika nahodha wa St Louis Bertrand Esther aliisawazishia timu yake baada ya kufunga kwa kichwa akitumia vema makosa ya walinzi wa Yanga waliochelewa kujipanga

Mara baada ya kusonga mbele Yanga sasa itakutana na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudan na Township Rollers ya Botswana, ambapo katika mchezo wa kwanza Township Rollers waliibuka na ushindi wa mabao 3-0

St Louis iliwakilishwa na Michael Ramandimius, Jean Paul, Steve Henriette, Damien Maria, Bertrand Esther, Travis Laurence, Herve Rakotoarison, Tahiry Adriamandiby/ Jude Nancy dk 56, Mervin Merthiot/ Roddy Malanie dk 57, Ellijah Tambo, na Karl Hall

Yanga sc Youth Rostand, Hassan Kessy, Gadier Michael/ Hajji Mwingi dk 76, Nadiri Haroub ” Canavaro” Kelvin Patrick Yondan, Pato Ngonyani, Said Juma/ Raphael Daud dk 60, Papy Kabamba, Pius Buswita, Ibrahim Ajib na Emmanuel Martin

Sambaza....