Sambaza....

Klabu ya Yanga watakuwa wanamkaribisha Al Hilal katika dimba la Benjamini Mkapa huku wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa katika mashindano ya klabu bingwa Afrika msimu wa 2022/23 na kudondokea shirikisho hivyo ni haki yako kuhakikisha wanamgalagaza Al Hilal hiyo.

Mchezo huu utakuwa wenye mvuto mkubwa sana, sio tu ndani ya Tanzania hata nje ya mipaka ya Tanzania(Afrika).

Mvuto wa mechi hii unachangiwa na vitu vingi sana lakini kandanda.co.tz imekuandalia vitu vichache ambavyo vitaufanya mchezo huu kuwa wamoto kweli kweli. Vitu hivyo ni÷

■ Yanga kuwa na matokeo mabovu ya hivi karibuni katika mechi zake mbili za mwisho ambapo alipoteza goli moja kwa bila dhidi ya waoka mikate wa Chamazi (Azam) kisha akafungwa tatu kwa moja na wafuga nyuki wa Tabora (Tabora United). Yanga hawatakubali kuendelea kupoteza kwani presha toka kwa mashabiki ni kubwa sana hivyo watapambana kushinda.

■ Ujio wa kocha mpya. Hivi karibuni yanga wamemtambulisha SEAD RAMOHIC kama kocha wao mpya baada ya kumtupia vilago Muargentina Miguel Gamondi. Watu wanatamani kuona kocha mpya atakuwa ameibadilishaje Yanga katika mda mdogo aliokuwa na timu.

■ Rekodi ya msimu uliopita klabu bingwa Afrika. Msimu wa mashindano ya CAFCL ulioisha Yanga walifanikiwa kufika robo fainali na kutolewa na Mamelod Sundowns ya Afrika ya Kusini kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Msimu huu yanga wanaitamani rekodi waliyoiweka hivyo mchezo huu unakwenda kuanzisha NDOTO.

Na kama yanga ataanza vizuri katika mchezo huu basi watakwenda kurudisha ile hali iliyopotea (ushindi) kwani hadi sasa hivi hali ya yanga bado iko chini na mchezo pekee wa kurudisha hali hiyo ni dhidi ya al hilal.

■ DUBE DAY. Yanga wameamua kuipa jina siku ya mchezo wao dhidi ya Al Hilal kuitwa DUBE DAY. Hii ni moja kati ya sababu muhimu inayoufanya mchezo huu uzidi kuwa na mvuto kwani ni mzigo kwa prince Dube. kila mmoja anaamini prince Dube ni mchezaji mzuri na anaweza kuwavusha hapa. Lakini pia Dube anapitia kipindi kigumu kutokana na kiwango chake kupungua katika kufumania nyavu.

Hivyo yanga wanataka kutuaminisha kuwa Dube anakiwango kizuri na ni mchezaji mzuri na yote yaliyopita ni sehemu tuh ya changamoto za kimpira. Lakini pia hii inatupa taswira ya kuwa mchezo huu unakwenda kumfungua prince Dube na kurudisha makali yaliyopotea.

Je mchezo huu utakwenda kumrudisha Dube aliyepotea? Majibu tutayapata pale Benjamini Mkapa. Kuna umuhimu mkubwa wa Yanga kushinda mchezo huu. Huu ni mchezo wa kufa na kupona na ni mchezo wa kujimaliza kwa yanga kuhakikisha wanashinda.

HEBU FIKIRI KAMA YANGA WATAPOTEZA MCHEZO NINI KITATOKEA?

Sambaza....