Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba bado hali si shwari kutokana na matokeo mabaya waliyokutana nayo katika michezo yao ya Ligi Kuu ya NBC na hivyo kupelekea viongozi wake kufanya tathmini ya usajili wao mkubwa walioufanya.

Katika michezo mitatu ya mwisho Simba imekua na muenendo mbovu ambapo wamepata ushindi mara moja, sare moja na kipigo kimoja kizito kutoka kwa Watani wao cha mabao matano.

Kufuatia hali hiyo imewafanya viongozi wa Simba chini ya Mwenyekiti wake wa bodi Salim Abdallah “Try again” kupitia usajili wao na kukiri kuna wachezaji wataachana nao dirisho dogo.

Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya Simba Salim Abdallah.

“Baada ya matokeo tuliyopata siku za karibuni tumefanya tathimini ili kuona tumekwa wapi na tumegundua wachezaji wengi hawajitumi,” alisema na kuongeza “Tumewaambia hatuta wavumilia kila mmoja anapaswa kujituma.”

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa lakini mpaka sasa wanaonekana kutokuisaidia Simba ni pamoja na Willy Onana, Aubirn Kramo, Ayoub Lakreb, Abdallah na Hussein Kazi. Wengi wao wakiwa wamepata dakika chache kucheza na pia kushindwa kabisa kuitumikia Simba katika mchezo wa ushindani.

Mwenyekiti pia ametanabaisha mipango yao kuelekea dirisha dogo la usajili akikiri watafanya usajili tena ili kukipa nguvu kikosi chao kuelekea michuano ya kimatafa Afrika na Ligi za ndani.

Ayoub Lakred.

“Tutasajili lakini kwa mapendekezo ya mwalimu mpya ambaye tutamtangaza karibuni.”

“Unajua unaweza kumsajili mchezaji hata kutoka Al Ahly lakini akaja hapa na kocha asimtumie, tutampa jukumu hilo yeye kwakuwa ndiye anajua anataka mchezaji wa aina gani kwenye kikosi chake,” amesema Try Again.

Sambaza....