Sambaza....

Kocha wa zamani wa Moroka Swallows na Kaizer Chiefs Ernst Middendorp amechagua makocha watatu kutoka Afrika Kusini ili kuungana nae katika benchi lake la ufundi katika klabu ya Singida Fountain Gate FC.

Kocha huyo wa Mjerumani alitambulishwa kama kocha mkuu mpya siku ya Ijumaa, wiki mbili tu baada ya kujiuzulu kwa kushtukiza katika klabu ya SV Meppen ya Ujerumani.

 

Hata hivyo, Middendorp hakuwa na kazi kwa muda mrefu na safari yake iliyofuata inampeleka kwenye mpango huo kabambe wa Singida Fountain Gate FC. Lakini amezungukwa na nyuso zinazojulikana, hii ni kwa mujibu wa mtandao mmoja wa huko Afrika Kusini.

Mjerumani huyo atamchukua Thabo Senong kuwa kocha msaidizi, Kelvin Ndlomo na Thembalethu Moses atakuwa kocha wa makipa.

Senong anajulikana zaidi kwa kazi nzuri aliyoifanya kama kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini walio chini ya umri wa miaka 20 akiiongoza kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2017, wakati pia alifanya kazi kama msaidizi wa Bafana Bafana wa Shakes Mashaba.

Singida Fountaine Gate ilitangaza kuachana na kocha Hans Plujim mara tu baada ya kufuzu raundi inayofuata ya kombe la Shirikisho Afrika walipowatoa JKU ya Zanzibar.

Sasa kocha huyo Mjerumani ana kibarua chakuwavusha Singida katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Future Stars ya Misri.

Sambaza....