Sambaza....

Theo Walcott ametangaza kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 34 akiitumikia Southampton ya Uingereza.

Winga huyo wa zamani wa Arsenal, Everton na Southampton alimwambia Gary Neville kwenye podcast ya The Overlap kuwa uamuzi huo ni “wa kushangaza” lakini “anataka kujaribu mambo mapya”.

Walcott anastaafu kucheza Kandanda na kuhitimisha miaka yake 23 ya maisha yake ya kandanda England ambapo alicheza mechi 397 za Premier League.

“Nitakuwa nikitundika buti zangu rasmi. Inatisha sana, siwezi kusema uongo,” alisema Walcott.

“Inasikitisha kwa sababu soka ndilo pekee nililojua tangu nikiwa na umri wa miaka 16 au hata chini yake. Nataka kujaribu mambo mapya ambayo sikuwahi kuyapitia nikiwa mtoto, nilikosa mengi.

Theo Walcott.

“Ninahisi tu kama nataka kupata uzoefu wa maisha – mambo [kawaida] yanayohusu soka kwangu.”

Katika kipindi chake cha miaka 13 akiwa na The Gunners, Walcott alishinda vikombe vitatu vya FA pamoja na Ngao mbili za Jamii.

Theo.

Pia Walcott amezitumikia kwa nyakati tofauti timu za Taifa za England. Ametizumikia timu za vijana za U-16, U-19 na U-21, huku pia ile ya wakubwa (Three Lions) akicheza michezo 47 na kufunga mabao nane.

Alipata umaarufu mwaka wa 2006 akiwa na umri wa miaka 17 alipochaguliwa katika kikosi cha Sven Goran Eriksson cha Kombe la Dunia cha Uingereza nchini Ujerumani.

Sambaza....