Sambaza....

Wapwa, anaitwa Pacome Zouzoua ikitamkwa ‘zuzwaa’ pamoja na kupata muda mchache wa kucheza katika derby ya Kariakoo Mkwakwani alionyesha jambo.

Kuna kitu kikubwa alikionesha juu ya uwezo wake hasa kwenye mbinu na uwezo wake wakiufundi ikiwemo kuunganika na mwenzake (ushirikiano)

 

Mikimbio yake na “anticipation” yake ilikuwa poa, hii inaashiria mambo yamo ikiwemo usahihi wa pasi kucheza na mpira na bila mpira.

Kujiamimi  kwake hakukuwa kwa 100% yawezekana ukubwa wa mechi na ugeni wake ilisababisha hali hiyo hivyo itabidi tumsubiri baadaye huko mbele tumuone.

Kwenye upigaji wa penati alipoteza lakini licha ya kile kinachoelezwa golikipa alikuwa anatoka mapema lakini yeye alipaswa kusoma na kuheshimu ubora wa Ally Salimu kwa kuwa wenzake wawili walipiga upande ule na hawakufunga.

Pacome Zouzoua.

Maana yangu alipaswa kupiga upande mwingine na mara nyingi makipa wengi wapo vizuri upande wa kulia kwa maana wanapolaza mkono huo kisha kushoto kuwa juu.

kwa hapa unaweza kumuhukumu kwenye kuusoma mchezo, nitamsubiri kwenye mechi nyingine kisha nitakuja na maoni ya ujumla.

Sambaza....