Muda wa PSG kukubali hizi zama zipite ndio huu, wamefanya kila kitu lakini imeshindikana ndani ya Ulaya. Kuanzia kuleta majina makubwa ya wachezaji mpaka kubadili makocha kila msimu.
Ligi Kuu ya Ufaransa wameshinda sana ubingwa na hawana sana uhitaji nayo kama UEFA Champions League! Kombe la Ligi wameshinda sana na sasa wanahitaji UEFA Champions League basi.
Wameleta majina makubwa lakini imekuwa tofauti ndani ya Klabu. Kuanzia kwa Kylian Mbappe ambaye amekataa kuuzwa na kuongeza mkataba wake ili aondoke bure mpaka kwa Neymar JR ambaye imeripotiwa naye anataka kuondoka.
Nasser Al-Khelaifi muda huu lazima akubali kwenda bila haya majina makubwa sababu huenda yanachelewesha sana mipango yao. Lionel Messi na Sergio Ramos wameenda pale pia lakini bado ikawa ngumu kuchukua ubingwa wa Ulaya.
Pesa nyingi sana zimetumika kulipa mishahara ya mastaa hao ukiunganisha na ada zao za usajili ni fedha nyingi sana lakini ubingwa wa Ulaya bado haujaletwa Paris, inabidi zama zibadilike.
Msimu huu amekuja Luis Enrique ambaye ana uwezo wa kutengeneza timu kupitia majina ya wachezaji wa kawaida na waliosajiliwa kwa pesa ndogo na akakupa matokeo bora sana uwanjani.
Naamini! Luis Enrique kama hatopewa presha kubwa basi huenda akafanya vizuri sana barani Ulaya kupitia wachezaji alionao bila haya majina makubwa.
Huu ni muda wa Nasser Al-Khelaifi ambaye ni Rais wa PSG kukubali mabadiliko yao ya muundo wa timu kupitia kwa Neymar JR na Kylian Mbappe.