Sambaza....

Wapwa, siku zote sio mbaya kuiga kitu kizuri ambacho mwenzako ameanzisha na ukakiendeleza au kufanya kwa sehemu yako pia! Singida Fountain Gate FC wamefanya hivyo.

Vizuri, Simba walianzisha hii njia ambayo pia wengine wamekuja na wanafanya kwa upande wao, sasa ni mara ya pili mfululizo linafanyika pale uwanja wa Liti, Singida.

Ilikuwa Singida Big Stars kwa mwaka jana kabla ya jina kubadilika na kuwa Singida Fountain Gate FC kwa mwaka huu! Ndio, imebadikika sehemu ndogo tu ya uongozi na wazo limebebwa linaendelea kuishi kama kawaida.

Timu yao ipo vizuri sana tangu imepanda Ligi Kuu, kila sehemu inacheza kwa upande wake na majukumu yake ndani na nje ya uwanja. Kuanzia miundombinu ya timu kama usafiri, uwanja na hata wachezaji ambao wapo Klabuni.

Winga Dickson Ambundo akimuacha mlinzi wa AS Vita.

Singida wamekuja msimu uliopita wakaingia moja kwa moja ndani ya nne bora ya Ligi Kuu na msimu ujao watashiriki michuano ya Kimataifa ya vilabu kwa upande wa Shirikisho ( CAF Confederation Cup ).

Kama watakuwa na muendelezo mzuri wa tamasha lao basi baada ya miaka mitano watakuwa mbali sana, na iwapo tu wataweza kuendelea kulinda ubora walionao ndani ya uwanja kwa hapa walipo au zaidi kwa baadae.

Kiungo Mourice Chukwu akipiga  pasi mbele ya mchezaji wa AS Vita katika siku yao.

Sio kila timu inaweza kufanya hivi ambavyo wamefanya Singida Fountain Gate FC ndio maana wamezikuta klabu nyingi ambazo zina muda mrefu sana kwenye Ligi Kuu na hawakuwahi kufanya tamasha kama hilo.

Hii ni kubwa sana na itazidi kuwa kubwa zaidi kama wataendelea kufanya hiki ambacho wanafanya ndani ya klabu yao, vyema zaidi klabu nyingine zikafanya hivi sababu inasaidia sana kuiuza timu kwa wapenzi wa soka na wale wapya ambao wameanza kuvutia na mchezo huu. Hongera sana Singida Fountaine Gate.

 

Sambaza....