Sambaza....

Fahari ya Tanga ni mapenzi na ukarimu wao lafudhi ya lugha yao ndio kivutio kingine madaha majivuno kwa mbali ndio asili yao bila kusahau mapango ya Amboni ni sehemu ya vivutio muhimu sana kwao.

Mgawanyiko wa namba za mitaa ni jambo la kushangaza zaidi ukiachana na hayo yote kuna fahari ya Tanga, fahari ya Watanzania hapa namzungumzia Champez one Time Hassani Mwakinyo.

Mwakinyo ni moja ya mabondia bora sana kwenye nchi yetu, majivuno ya watu wa Tanga ni moja ya silaha zake. Lakini pamoja na majivuno yake haiondoi jebu inayouma kwenye mwili wa binadamu aliechagua ngumi kuwa sehemu ya ajira yake lakini Light inatesa kwenye miili ya wenzake huku yeye akifurahia hayo.
Champez alikuwa kimya baada kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith nchini Uingereza katika mazingira tata. Lakini mwaka huu mwezi wa nane Champez anarejea kwenye pembe nne za ulingo kuwania mkanda wa WBO ndoto inaenda kuwa kweli hii ni ndoto ya mabondia wengi duniani inaenda kutimia kwa Champez.

Champez ni ndoto ya Watanzania wengi lakini chini ya Dunia yake huku akikataa kuwa daraja la mabondia wengine. Moja ya kauli ngumu kwa Mwakinyo ni kutopigana kwa sababu ya hamniwezi, kwa maana mapambano yasiyo na faida nae huku akiwa hajui anapata nini  kwenye hilo pambano.

Moja ya takwa ili kupigania mkanda huo anaokwenda kuupambania Champez ni bondia kutopoteza mapambano zaidi ya matano. Champez na Dunia yake, mabondia wa Tanzania na Ulimwengu wao, hii ndio tofauti ya wao na yeye na kiburi chake cha Kidigo.

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Champez.

Abuu Mwakyoma.


Sambaza....