Aliyekua kocha wa Yanga amekosa kibarua cha kuifundisha timu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini waliyokua katika mazungumzo ya muda mrefu na klabu hiyo imemtambulisha Molefi Ntseki.
Klabu ya Kaizer Chiefs imemteua Molefi Ntseki kama kocha mkuu mpya, akichukua nafasi ya Arthur Zwane kabla ya msimu wa 2023/24 wa DStv Premiership.
Zwane, ambaye aliteuliwa kuwa kocha mkuu mwezi Juni 2022, sasa atahudumu kama kocha msaidizi wa kocha huyo wa zamani wa Bafana Bafana.
Nasraddine Nabi sasa anapaswa kuangalia kibarua kingine kwani kipaumbele chake kilikua kujiunga na wababe hao wa Soweto ili kurejesha ufalme wao mbele ya Mamelodi Sundowns.
Inaaminika miongoni mwa sababu zilizowafanya Chiefs na Nabi kushindwa kuelewana na ni moja ya sharti la Nabi kutaka kwenda na wasaidizi wake kitu ambacho mabosi wa Amakhosi hawakua tayari.