Sambaza....

UONGOZI wa KMC umeanza mazungumzo ya kimya kimya ya kumrejesha aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo, David Bryson ambaye mkataba wake aliosaini wa miaka miwili na Yanga unafikia tamati msimu huu.[Mwanaspoti]

Klabu ya Cotton Sports ya Cameroon inahitaji kiasi cha dola 150,000 kwa Simba ili kumuachia beki wake wa kati Che Fonde Malone [Nuhu Adams]

Uongozi wa klabu ya Azam umesema wala hauna mpango na winga Benard Morrison, winga huyo kutoka Ghana tayari ameachana na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika [Champion]

Benard Morrison

Kalidou Koulibaly amejiunga na Al Hilal ya Saudi Arabia na kuachana na Chelsea aliyoichezea msimu mmoja pekee akitokea Napoli ya nchini Italy. [Skysports]

Al-Nassr wanatumai kukamilisha dili la winga wa Chelsea kutoka Morocco Hakim Ziyech, 30, mapema wiki hii, na kumfanya kuwa mchezaji wa nne kuondoka Stamford Bridge kwenda Saudi Arabia msimu huu wa joto. [Fabrizio Romano]

United inamtazama kiungo wa kati wa Ajax na Ghana Mohammed Kudus, 22 baada ya kushindwa kumpata Mousen Mount wa Chelsea. [ESPN]

Mohamed Kudus

Nasraddine Nabi huenda akatambulisha ndani ya masaa 48 kutokea sasa baada ya yeye mwenyewe kukiri wapo katika hatua za mwisho za kukubaliana na Kaizer Chiefs [The South African]

 

Sambaza....