Kufuatia matatizo ya kimkataba kati ya Feisal Salum na Klabu yake ya Yanga kiungo huyo wa Zanzibar amesema hana shida na Yanga ila shida ipo kwa rais wa Klabu hiyo Hersi Said.
Fei Toto amesema hajaondoka yanga kwasababu ya kuwa ugomvi na Yanga ama mashabiki wake hapana, kilichomuondoa yanga raisi wa klabu hio. Akiongea na kusikika katika kipindi cha redio cha Clouds fm amesema “Yanga ni taasisi kubwa sana, Yanga ni timu kubwa sana na mimi mwenyewe nina mapenzi na Yanga, sina ugomvi na Yanga, sina ugomvi na wanachama. Wanaaminishwa kuwa mimi ni mbaya lakini mimi sina ugomvi nao, nawapenda kama wanavyonipenda.”
“Mimi tatizo langu kubwa ni Rais wa timu na ndio maana wakati nakaa nae chini nikamueleza na nikamwambia naomba tukae tumalize kila mmoja afanye mambo yake,” aliongezea Feisal.
Inaaminika kuwa moja ya sababu ya Feisal kutofautiana na Rais wa Klabu ni kurubuniwa katika utiaji saini wa mkataba kwani Feisal alikubaliana kusaini mkataba wa miaka miwili na Yanga lakini Rais wa Klabu akaandika na kuwa miaka mitatu na ilifanyika bila Feisal kujua.
“Nimekukosea nisamehe Rais aliniomba na mimi nikamwambia sawa nimekusamehe lakini naomba niache nikatafute maisha yangu,” alisema
Licha ya feisal kumsamehe lakini imeshindikana kuvunja mkataba na kuondoka Yanga kiwepesi na kupelekea mgogoro uendelee kulindima kati yao, anachotaka Feisal ni kuondoka Yanga hataki tena kuendelea kuwatumikia Yanga licha ya kutokua na ugomvi Klabu.