Sambaza....

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele huenda akaonekana katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu ujao kutokana na kuhitajika na wababe wa nchini humo Kaizer Chiefs.

Mayele amekua na kiwango kizuri tangu ahamie Yanga akitokea AS Vita ya nchini kwao Congo kutokana na kasi yake ya ufungaji mabao na kupelekea mafanikio makubwa kwa Klabu yake ya Yanga.

“Kaizer Chiefs wametuma maombi juu ya uwezekano wa mazungumzo ya ufunguzi yakumsajili lakini hawajatoa ofa rasmi. Tulikuwa na timu ambayo imependekeza kutoa dola nusu milioni na nina uhakika kwamba tunaweza kupata zaidi kwa ajili yake ikiwa tutashikilia zaidi,” chanzo kiliuambia mtandao wa Kickoff Magazine.

Fiston Mayele

Chanzo hicho pia kilisema si tu Fiston anahitajika Afrika Kusini lakini pia kuna baadhi ya timu kutoka nchi za Kiarabu zimeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo kutoka Congo DR.

“Al Hilal pamoja na wapinzani wao El-Merreck pia wameonyesha nia ya kumuhitaji lakini pia kuna klabu moja ya nchini Uturuki pia imekua ikimfwatilia. 

Raja Casablanca pia walionyesha nia yao pamoja na Zamalek lakini wao bado hawajatuma ofa rasmi,” kiliongeza chanzo hicho.

Mpaka sasa Fiston Mayele amefunga mabao 16 katika Ligi Kuu ya NBC huku pia akifunga mabao matano katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabao saba aliyoyafunga katika raundi za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sambaza....