Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga maarufu kama Wananchi leo wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa jioni leo katika Uwanja wa Chamanzi.

Ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Dodoma Jiji umewafanya Yanga kubeba alama tatu na kufikisha alama 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika Ligi. Simba wanaoshika nafasi ya pili wana alama 67 na wakishinda michezo yao miwili iliyosalia watakua na alama 73.

Wananchi walistahili ubingwa huo na kutetea taji lao walilolichukua msimu uliomalizika  kutokana na kiwango kizuri walichoanza nacho msimu huu licha ya kupoteza rekodi yao yakucheza bila kufungwa “unbeaten” mbele ya Ihefu.

Mpaka kufikia mchezo wa leo Yanga imepoteza michezo miwili na kutoa sare mbili pekee wakionyesha ni timu iliyokua na ubora kiasi gani na ikistahili pia kutwaa ubingwa katika Ligi Kuu ya NBC.

Pia mpaka kufikia mchezo wao wa 28 wa Ligi Yanga imefanikiwa kufunga mabao 56 wakizidiwa na Simba pekee (wenye magoli 66) huku ikiwa imefungwa mabao machache zaidi wakiwa sawa na Simba (mabao 15) ikiwa imesalia michezo miwili kwa Ligi kumalizika.

 

Sambaza....