Sambaza....

Klabu ya Yanga, inaelekea kutawazwa kuwa mabigwa wa Ligi Kuu Kuu Tanzania Bara. Mtandao wako wa kandanda unakuangazia rekodi zinasemaje kuhusu ligi Kuu Tanzania bara kuanzia msimu wa 2017-18.

Katika misimu sita iliyopita ikiwa pamoja na mwaka huu, klabu ya Simba imejivunia zaidi ya alama 457 na magoli 398 katika michezo 196 (Bado Msimu huu haujaisha). Takwimu hizi zinaifanya klabu hii kuwa Five Star klabu ya Kandanda.

klabu ya Yanga kwa misimu yote imekuwa haina uwezo mkubwa wa kufunga mabao. Hata pale ambapo imekuwa ni bingwa, haikuweza kutoa mfungaji bora. Kwa kipindi cha miaka hii sita, na sasa iikiwa imebakiwa na michezo miwili. Yanga imevuna alama 432 na kufunga mabao 287, asilimia 41 ya mabao yaliyofungwa na watani hawa.

Msimu wa 2022/2023 licha ya kwamba Simba itashika nafasi ya pili lakini pia imefunga mabao mengi zaidi (62 kwa 50). Na imemtandika Yanga katika mechi ya msimu huu.

Mafanikio ya Simba kwa nyakati zote hizi inachukua ubingwa, imeifanya klabu hii kuwa na ‘maturity’ ya hali ya juu, ikiwa na kufikia hatua ya robo fainali klabu bingwa mara nne. Kuongeza alama za ushiriki wa timu kimataifa za Tanzania, hakika ni matunda ambayo hizi alama zinaweza kuongea kwa nguvu zaidi.

Yanga butu, hata pale George Mpole alipoibuka mfungaji bora wa Ligi, hakuweza kuvunja rekodi ya waliomtangulia. Mayele anaenda kuwa mfungaji magoli kwa magoli chini ya 18, ambao Kagere na Okwi walikuwa moto kipindi hicho.

Yanga Bingwa, ila Simba ni Baba Lao. Na hakika, kimtaani mtaani Simba anatakiwa kumcheka Yanga sana. Lakini sababu ni biashara, ni muda muafaka kwa Yanga kuandaa tukio la kumcheka mtani wake.

Sambaza....