Wananchi Yanga leo wanashuka dimbani kuvaana na Rivers United katika mchezo wakwanza wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika katika mchezo utakaopigwa saa kumi jioni kwa saa za Tanzania.
Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga Nasradine Nabi amesema “Hongera kwa uwanja mzuri, niwapongeze pia uongozi wa Yanga kwa kuhakikisha tumekuja mapema hapa Nigeria hali ya hewa na nzuri na tumekua na maandalizi mazuri.”
Pia Nabi ameongeza Wao kama Yanga wanawaheshimu wapinzani wao licha ya kuongoza kundi lao huku wakiwa tayari kupigania ndoto zao za kwenda nusu fainali.
“Hatujioni wakubwa kwasababu tumeongoza kundi. Tunawaheshimu sana wapinzani wetu lakina malengo yetu ni kuhakikisha tunafika nusu fainali,” alisema Nabi
Nae kiungo wa pembeni wa Yanga Benard Morrison akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema hawakwenda Nigeria kujifurahisha wanataka kushinda mchezo huo
Benard Morrison “Malengo yetu ni kuiwakilisha Yanga na Tanzania vyema kwa ujumla. Hatuko hapa kwasababu yakujifurahisha, tuko hapa kwaajili ya kupata matokeo mazuri.”
Yanga wanakwenda nchini humo wakiwa wamebeba kisasi kwani mwaka 2021 walitolewa na Rivers United baada ya kufungwa michezo yote miwili nyumbani na ugenini kwa jumla ya mabao mawili kwa sifuri.