Sambaza....

Na Charles Abel

Inawezekana ni kweli Aucho hakuwa na siku nzuri juzi dhidi ya Simba lakini siafiki kusema kuwa kama Yanga inataka kushindana katika level za juu haipaswi kumtegemea.

Labda jicho lake la ufundi limeona hivyo lakini kwa mtazamo wangu, Aucho mechi moja ya jana haipaswi kumshusha Aucho kiasi hicho.

Huyu ni mchezaji ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa Yanga ifike hatua ya makundi na hata kuongoza na kutinga robo fainali kwa nini?

Khalid Aucho.

Hoja yangu itasimama kwenye takwimu zaidi, kwa mujibu wa mtandao wa Fotmob, huyo Khalid Aucho kwenye hatua ya makundi ndiye mchezaji wa safu ya kiungo ya Yanga mwenye takwimu nzuri za upigaji tackling ambapo kati ya tackling 7, tackling 6 alizifanya kwa usajihi sawa na 85.7% akifuatiwa na Mudathir Yahya mwenye 71.4% lakini ndiye aliyeongoza kwa usahihi katika kushinda mipira ya juu (aerial duels) ambapo kati ya mapambano manne ya mipira ya juu alishinda nusu yake.

Aucho alikuwa na wastani wa kufanya recoveries 8 na interceptions 5 na clearance 1 kwa mechi huku akipiga idadi ya pasi 341 .
Sifa kubwa ya kiungo mzuiaji ni kuilinda safu yake ya ulinzi isifikiwe kirahisi na wapinzani na hapo Aucho amefanikiwa ninaweza kusema.

Katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga iliruhusu mabao manne ambayo yote yalitokana na mipira ya kutenga na sio open play, means Aucho kama kiungo mzuiaji alitimiza jukumu lake la msingi.

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho akimuacha Clatous Chama wa Simba.

Kutofanya vyema Derby inawatokea wachezaji wengi tu na tumewahi kulishuhudia hilo lakini isitoshe kuwa fimbo ya kumchapia Aucho ambaye hapana shaka ni miongoni mwa viungo bora hapa nchini kwa sasa.

Tuwahukumu kwa haki hawa wachezaji jamani. Aucho huyu tunayesema Yanga isimtegemee katika level za juu ndiye miongoni mwa waliochangia ifike hapo juu kwenye Kombe la Shirikisho.

Au robo fainali sio hatua ya juu?

MZEE WA GHAFLA

Sambaza....