Sambaza....

Tayari droo ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imepangwa jana usiku na tayari Wananchi Yanga wamemjua mpinzani wao anaefuata katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.

Yanga wamepangwa kukutana na Rivers United ya nchini Nigeria katika robo fainali na kukumbushia timu hizo mbili zilipokutana msimu uliopita na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga wameonekana kufurahia droo hiyo.

 

Kwa upande wa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele yeye baada ya droo hiyo amefurahia na anawasubiri kwa hamu Wanaijeria hao kwani hakupata nafasi ya kukutana nao mara ya mwisho walipocheza dhidi ya Yanga.

Mayele amesema sasa ni wakati mzuri wa kulipiza kisasi na kuwaonyesha wao ni kina nani kwani baada ya kutolewa nao mwaka jana watu waliongea sana.

Mara ya mwisho Yanga kukutana na Rivers walikubali kichapo cha bao moja bila katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

“Mimi binafsi nilikuwa namtaka kwasababu mwaka jana sikupata nafasi ya kucheza naye, tulitolewa mapema watu wakaongea sana kwahiyo tumempata sehemu nzuri,” alisema Fiston Mayele.

Yanga itaanzia ugenini kati ya April 21 na 23 nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza kabla ya kurudiana nao Rivers kati April 28 na 30 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Sambaza....