Sambaza....

Kufuatia kipigo cha mabao matatu kwa moja walichokipata Simba kutoka kwa Raja Casablanca kocha wa Simba amesema licha ya kipigo hicho lakini timu yake inazidi kuimarika.

Kocha huyo Mbrazil Robert Oliveira amesema ingawa wamefungwa mabao matatu kwa moja lakini anaona maendeleo katika kikosi chake na watazidi kuwa tishio mbeleni.

 

Robert Oliveira “Nina muda wa miezi minne hapa lakini hii timu itakuwa imara zaidi siku chache zijazo. Timu inacheza vizuri ikiwa na mpira na hata isipokuwa nao.

Nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza vizuri ingawa tumepoteza kwa mabao matatu, ilikuwa mechi nzuri Raja ni timu bora.”

Kufuatia kipigo hicho kutoka kwa Raja klabu ya Simba sasa imepata ushindi katika michezo mitatu pekee kwenye kundi lao huku ikifunga mabao kumi na kuruhusu mabao saba.

Kiungo wa Simba Saidoo Ntibazonkiza akitafuta mbinu zakumuacha mchezaji wa Raja Casablanca.

Simba sasa wanarudi nyumbani kuendelea na michezo michezo ya Ligi Kuu ya NBC pamoja na kombe la FA ambapo wanakabikiwa na kibarua kigumi mbele yao kwa kucheza michezo miwili mfululizo dhidi ya “Mbogo maji” Ihefu Fc.

Simba wataanzia nyumbani Uhuru Aprili saba mwaka huu katika michuano ya FA dhidi ya Ihefu kabla ya kurudiana nao tena ikiwa sasa ni katika mchezo wa Ligi siku nne mbele katika uwanja wa Mbarali Mbeya safari hii Ihefu wakiwakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Sambaza....