Kocha mkuu wa Uganda the Cranes Milutin Sredojevic ‘Micho’ kuelekea mchezo wa kesho wa marudiano dhidi ya Stars ameonyesha wasiwasi wake kutokana na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na walinzi wa timu hiyo ya Tanzania.
Micho kocha wa zamani wa Yanga ameyaongea hayo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kufuzu Afcon nchini Ivory Coast mapema mwakani.
“Ni vigumu kufanya mabadiliko dhidi ya timu yenye nidhamu kubwa kwenye kujilinda, timu ina walinzi watatu wa kati ukiongeza na Novatus (Dismas), ukiongeza Himdi Mao na Mudathir Yahya. Ilikuwa ni vigumu kwetu kuvunja ukuta huo na sasa kuna ongezeko la Shomari (Kapombe) na Tshabalala (Mohammed Hussein).” Milutin Sredojeciv alisema
Kuelekea mchezo huo Uganda wanahitaji ushindi ili kufufua matumaini yao ya kufuzu michuao hiyo ya Afcon. Kupoteza ama sare kutawafanya kuondolewa rasmi katika kinyang’anyiro hicho cha kufuzu.