Kuelekea mashindano pendwa ya Ramadhani Cup msimu huu kutakua na mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo kati ya Silent Ocean na Wanahabari za michezo utakaopigwa katika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park.
Michuano hiyo ya Ramadhan ambayo huwa mahususi katika mfungo wa Ramadhani inaanza rasmi kesho kwa mchezo kati ya Silent Ocean na Mr Discount Center utakaoanza saa nne na nusu usiku.
Kabla ya mchezo huo kutakua na mchezo wa ufunguzi ambao utawakutanisha wafanyakazi wa Silent Ocean dhidi ya Timu ya mpira ya Wanahabari wa michezo. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kutokana na rekodi nzuri ya timu ya Wanahabari ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote.
Katika kunogesha shughuli hiyo mgeni rasmi atakua ni Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Hamia Mwinjuma huku kiasi cha miliono tano kikitolewa kwa mshindi wa mchezo huo na wadhamini wa michuano hiyo Silent Ocean.
Kuelekea mchezo huo nahodha wa Wanahabari Anuary Binde “Rais wa takwimu” amesema ni swala la muda tuu kwa kuchukua zawadi iliyowekwa katika mchezo huo.
“Takwimu zinaonyesha hakuna mechi Wanahabari waliwekewa kikombe na zawadi tukafungwa, kwaiyo nadhani ni vyema mkatukabidhi mapema leo kabla hata ya mchezo. Tutawafunga ndani na nje ya uwanja kesho” alisema Anuary Binde.
Nae nahodha wa Silent Ocean amesema mchezo wa kesho sio masihara watatumia nguvu na juhudi zote ili kupata matokeo hivyo Wanahabari waje wakiwa timamu.
Mrisho Karama ” Mchezo wa kesho sio wa masihara tumejiandaa tupo vizuri idara zote tunataka tuwaonyeshe tupo vizuri si tu kwenye kubeba mizigo mpaka uwanjani tupo vyema. Tunawaomba kesho mje kwa wingi katika mchezo huo kuna burudani yakutosha tena ukumbuke kuna milioni tano.”
Pia waratibu wa michuano hiyo mwaka huu Silent Ocean wamesema wamekuja kivingine zaidi wakihitaji kupata vijana waonyeshe vipaji vyao na pia zawadi kibao zitatolewa.
Idd Godigodi “Safari hii mashindano yatakua mazuri zaidi na kwa kiwango cha juu tutatoa nafasi zaidi kwa vijana ili waonyeshe vipaji vyao. Tutakua na zawadi nyingi, zawadi ya kipa bora, mchezaji bora, mfungaji bora kipa bora na timu yenye nidhamu.”
Michuano hii inategemewa kushirikisha timu 20 ambapo makampuni pekee ndio waliopewa nafasi yakushiriki michuano hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo chekundu Gerezani.