Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Amri Kiemba “Baba wawili” amesema haoni sababu ya kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Tanzania Adel Amrouche kuacha kumuita mshambuliaji kinda wa Yanga Clement Mzinze
Kiungo huyo wa zamani wa Simba amesema sio lazima aitwe aende akacheze lakini kuwepo kwenye programu za mwalimu ni kitu muhimu kwake. Kiemba ameyasema hayo alipokua katika kipindi cha Clouds Fm.
Amri Kiemba “Mwalimu mpya amekuja Walimu waliopo wanajaribu kumletea mradi wote, yeye ndio ataona yupo kwenye hali gani na ataweza akaanza naye vipi. Anaweza akaenda pale kufanya program zingine hata mechi asicheze sio kila anayeitwa atacheza mechi.
Mpango wa kuitwa timu ya Taifa ni mpana na ndio maana jana nilijaribu kusema kwa sababu ni mpango na Mzize anastahili kuwepo sio lazima aende akacheze na yeye ajihisi ni mpango wa timu ya Taifa.”
Kikosi cha Stars kimetajwa jana na kumekua na maoni tofauti ya wadau wa soka kwa kukosekana kwa baadhi ya nyota wanaoonekana kufanya vyema katika Ligi inayoendelea haswa kinda wa Yanga Clement Mzinze na wakongwe Mohamed Hussein, Shomary Kapombe na Salum Aboubakar “sure boy”.