Sambaza....

Wakiwa katika dimba la Benjamin Mkapa palipo na shangwe za Wananchi Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila mbele ya Real Bamako katika mchezo wao wanne wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Mwanzoni tuu mwa mchezo katika dakika ya nane alikua ni Fiston Mayele aliefunga bao na kupeleka shangwe jangwani baada ya kufunga bao safi akipokea mpira uliopitishwa na Musonda.

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Jesus Moloko baada ya makosa yaliyofanywa na mlinzi wa Real Bamako na hivyo kuifanya Yanga kupata ushindi wapili katika kundi lao.

Charlie Musonda.

Yanga watajilaumu wenyewe kwa kukosa ushindi mnene kwani Yanick Bangala alikosa mkwaju wa penati na hivyo kuinyima Yanga bao la tatu.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo US Monastir imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya TP Mazembe na hivyo kufikisha alama 10 wakiongoza kundi lao na Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama 7. 

Fiston Mayele.

Kwa mahesabu hayo Yanga ana nafasi kubwa yakufuzu kwenda robo fainali kutokana na kufanya vibaya kwa TP Mazembe na mpaka sasa wana alama tatu pekee.

Sambaza....