Sambaza....

Shirikisho la soka nchini TFF leo limetangaza kocha mkuu atakaekinoa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” baada yakukaa miezi kadhaa bila kocha mkuu.

TFF limemtangaza kocha Adel Amrouche mwenye miaka 58 raia wa Ubelgiji kuwa kocha mkuu wa Stars na kuchukua nafasi ya Kim Polsen alietimuliwa tangu mwaka jana.

 

Amrouche kocha wa zamani wa timu za Taifa za Kenya, Libya, Yemen na Equatorial Guinea ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika kutokana na kufanya kazi mda mrefu katika Bara hili.

Kocha huyo mwenye leseni ya Uefa Pro amevifundisha vilabu kadhaa vya Afrika kama USM Alger na MC Algier zote za Algeria na DC Motema Pembe alipopata mafanikio katika michuano ya Afrika.

Adel Amrouche

Mbelgiji huyo ni mkufunzi wa walimu wa Pro Lisence akifanya kazi na Shirikisho la soka Ulaya (UEFA). Lakini pia anaongea kwa ufasaha lugha za Kiarabu, Kingereza na Kiswahili na hivyo kuwa rahisi kuwasiliana na wachezaji wake.

Sambaza....