Sambaza....

Wachezaji wa Timu ya KMC FC wamereja kambini na leo kuanza maandalizi kuelekea katika mchezo unaokuja wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Januari 13 katika uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni imeingia kambini jana ikijiandaa na Mtibwa Sugar ambapo itakuwa ugenini na kwamba Kocha Mkuu Thierry Hitimana ambaye pia alikuwa Rwanda kutokana na kufiwa na mdogo wake pia ameingia na kuanza kukinoa kikosi hicho leo.

Ibrahim Ame.

Aidha katika kikosi hicho cha wana “Kino Boys” wachezaji wote wamerejea huku ikiwakosa wachezaji saba kutokana na sababu mbalimbali ambao ni Sadalah Lipangile, Ibrahimu Ame, Matheo Anton, Steve Nzingamasabo pamoja na Ismail Gambo ambapo wote ni kutokana na changamoto za kifamilia huku Emmanuel Mvuyekure na Hance Masoud wakiendelea kupatiwa matibabu kutokana na majeraha yamuda mrefu.

” Tumeanza mazoezi leo baada ya mapumziko mafupi ambayo tuliwapa wachezaji katika kipindi hiki ambacho Timu zipo kwenye mapumziko kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, kikubwa tunakwenda kwenye mchezo mgumu ambao tutakuwa ugenini na ndio mana tumekuwa na muda mfupi wakupumzika lengo likiwa kujiandae vizuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya.” Chiristina Mwagala msemaji wa KMC.

KMC wanakwenda kukutana na mchezo mgumu ambapo ukizingatia wanakwenda tena ugenini baada ya kutoka kupoteza dhidi ya Ihefu Januari tatu mwaka huu, lakini wanafurahi kuwa wachezaji wamerudi kwenye viwango vizuri hata kwenye mazoezi wanafanya wakiwa na hari na morali nzuri ambayo inaleta taswira njema kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

KMC FC inakwenda kwenye mchezo wa mzunguko wa 20 ikiwa kwenye nafasi ya tisa mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na jumla ya alama 22.

Sambaza....