Sambaza....

Mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika Yanga Afrika tayari wamewajua wapinzani wao katika michuano ya Kimataifa ambapo hatua ya makundi itaanza kutimua vumbi mwakani February.

Yanga Afrika imeangukia katika kombe la Shirikisho Afrika baada yakuondoshwa katika michuano ya Klabu bingwa Afrika na Al-Hilal ya Sudan kwa matokeo ya jumla ya magoli mawili kwa moja.

 

Yanga imepangwa katika Kundi D ya michuano ya Kombe la Shirikisho na timu kutoka Mali, Tunisia na Congo DR. Kundi la Yanga lina timu za TP- Mazembe (Congo DR), US Monastir (Tunisia) na Real Bamako kutoka Mali.

Yanga ina kila sababu yakufanya vyema na kusonga mbele kuelekea hatua ya robo fainali kutokana na timu walizopangiwa nazo. Huku wakichagizwa na uzoefu mkubwa wa wachezaji wake pamoja na ari kubwa waliyoipata baada ya kufika hatua hii kwa kuwatoa wababe kutoka Tunisia Club Africain.

Kwa upande wa klabu ya Simba Sc wao wapo katika michuano ya Klabu bingwa Afrika ambapo walikosa hatua hiyo ya makundi msimu uliopita baada ya kuangukia katika kombe la Shirikisho Afrika.

Simba wamerudi tena katika hatua ya makundi ya  msimu huu na sasa watakua katika Kundi C ambapo watafunga safari kuelekea nchi za Uganda, Guinea na Morroco. Simba imepangiwa Vipers ya Uganda, Horoya ya Guinea na Raja Casablanca ya Morroco.

Simba wamefika hatua ya makundi baada ya kuwaondosha Big Bullets ya Malawi na De Agosto kutoka Angola, ambapo Simba alipata ushindi katika michezo yote minne yaani nyumbani na ugenini.

Kwa kiasi kikubwa Simba ina nafasi yakusonga mbele na kuelekea robo fainali ya Klabu Bingwa kutokana na uzoefu mkubwa wa michuano hiyo licha ya kupangwa na vigogo kama Raja Casablanca na Horoya kutoka Afrika Magharibi.

 

Sambaza....