Klabu ya soka ya Polisi Tanzania imezindua jezi mpya watakazovaa kwa msimu 2022-2023 katika michuano yote watakayoshiriki msimu huu.
Polisi Tanzania wamezindua jezi tatu, jezi ya nyumbani, ugenini na jezi ya tatu (third kit) tayari kabia kuzitumia katika Ligi Kuu ya NBC na kombe la FA.
Kuelekea mchezo wao wa Ligi dhidi ya Simba utakaopigwa katika Dimba lao la nyumbani la Ushirika Moshi kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya uwanja huo kufungiwa kwa kukosa vigezo vyakutumika katika michezo ya Ligi Polisi Tanzania watatinga uzi huo mpya huku ikiwa ni kama ndio uzinduzi rasmi wa jezi hizo.
Polisi Tanzania watakua wenyeji wa Simba katika mchezo utakaopigwa November 27 mwaka huu katika Dimba la Ushirika Moshi katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC