Sambaza....

Mara baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa NBC Premier league ni wazi kwamba Yanga Africa atawakilisha nchi Kimataifa kwenye mashindano ya klabu bingwa ya CAF.

Hivyo basi atalazimika kuimarisha kikosi chake kwa Levo ya ushindani huo kwa kuwa huwa kuna utofauti mkubwa wa ligi ndani za ndani na zile za CAF.

Kwa kuwatizama mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga na kikosi chao kilichofanikisha ubingwa huo, ni dhahiri hakitoshi kwenye ushindani ujao upande wa CAF kama watakuwa na kusudio la kufanya vizuri.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Msimu 2021/2022.

Watalazimika kwenda sokoni kununua wachezaji wengine muhimu wenye angalau uwezo wa juu zaidi ikiwezekana na uzoefu wa kucheza michuano hiyo ya Afrika.

Lakini kabla ya kuangalia nafasi (position) muhimu kwa wachezaji wa wakuwasajili tuangalie wanaopaswa kubaki.

Binafsi naona wachezaji wa kigeni ambao wapo Yanga wapo wanaostahili kuondoka kupisha “quality” nyingine mpya akiwemo Makambo na Jesus Moloko huku nikiamini Chiko Ushindi anapaswa kubaki na kupewa muda zaidi wa kucheza.

Jesus Moloko wa Yanga akimtoka mlinzi wa Simba Mohamed Hussein “Tshabalala”.

Kwanini Chiko ushindi abaki na Jesus Moloko apishe?
Jibu langu ni moja tu Moloko amepata nafasi kubwa ya kucheza lakini amedhihirisha kuwa uwezo wake ( quality) yake ni ya kawaida sana sawa na wachezaji wengi wa ndani.

Hata ukiangalia takwimu zake na muda aliyopata nafasi ya kuwepo uwanjani haushabihiani hata kidogo.

Chico Ushindi (25) kulia akimtoka mlinzi wa Polisi Tanzania.

Na hii inawezekana kuchangiwa na sanaa yake ya uchezaji ya kizamani (pure winger) kukimbia mwisho wa uwanja kumimina krosi ndani.

Mawinga wa sasa hawakai ukingoni mwa uwanja muda mwingi wanacheza kama viungo wa kati na kukimbilia kwenye box ili kufunga moja kwa moja kitu ambacho yeye hakifanyi

Chiko Ushindi tangu siku ya kwanza namuona kule Arusha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni ambapo aliingia dakika za mwisho alikuwa na ujumbe fulani kiuchezaji.

Fiston Mayele (9) na Chico Ushindi (25).

Nilichogundua alikuwa hana utimamu wa mechi na yawezekana alikaa muda mrefu bila kucheza kabla ya kuja nchini.

Uwezo wake wa sasa unadhihirisha hili baada ya kuwa na utimamu wa mwili wake na amekuwa wa tofauti ni “winger dynamic”.

Anaweza kubadilika kadri ya eneo alilopo akafanya lile linalotakiwa kwa wakati husika, anajicho la goli na anamaamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

Chico Ushindi.

Bahati mbaya tu kachekewa kuikamata “form” yake hadi hapa mwishoni kwa maana hiyo ni mchezaji anayestahili kuwepo upande wa kimataifa na msimu ujao aweze kuonesha makubwa.

Moja ya sifa tofauti aliyonayo ni kupiga kwenye mwendo na uzito wa mashuti yake ni mkubwa sana ikiwemo shabaha ya goli ( target).

Akiongezewa hali ya kujiamini ni mchezaji wa maana kuendelea na Wananchi na kadri anavyozoea mazingira atafanya vyema kwenye ligi ya ndani na michuano ya CAF.

Sambaza....