Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Kim Polsen ametaja kikosi kitakachoingia kambini kujiandaa na michuano ya kufuzu Afcon ya 2023.
Katika kikosi hicho hakina sura mpya sana wengi ni wachezaji walewale walioitwa katika michezo ya mwisho ya Kirafiki iliyopigwa nchini katika kalenda ya FIFA dhidi ya Afrika ya Kati.
Katika kikosi hicho wamejumuishwa Salum Abubakar na Himid Mao ambao walikosekana mda mrefu, lakini kwa upande wa John Bocco yeye ameendelea kukosekana na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwenzake wa Simba Kibu Denis.
Taifa Stars itaingia kambini May 28 mwaka huu kujiandaa na michezo miwili dhidi ya Niger June 4 ugenini na mchezo wa pili dhidi ya Algeria utakaopigwa June 8 Benjamin Mkapa.