Sambaza....

Klabu ya DTB Fc imefanikiwa kupanda Ligi Kuu kwa msimu ujao baada ya leo kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa Ligi ya Championship dhidi ya Pamba katika uwanja wake wa nyumbani.

Juma Abdul mlinzi wa zamani wa Yanga ameiongoza timu yake ya DTB kuibuka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya Pamba ya Mwanza na hivyo kufikisha alama 65 ambazo haziwezi kufikiwa na vilabu vingine 14 isipokua Ihefu pekee mwenye alama 62.

Hongera DTB kwa kupanda Ligi Kuu ya NBC.

Mpaka sasa Ligi ya Championship imepigwa michezo 28 na kubaki miwili pekee ambapo DTB wana alama 65 wkaiongoza Ligi halafu wakifwatiwa na Ihefu nafasi ya pili wakiwa na alama 62 hivyo mpaka sasa tayari DTB amejihakikishia nafasi ya kupanda na kubakisha nafas8 moja pekee ambayo inagombaniwa na Ihefu mwenye alama 62 akifwatiwa na Kitayosce mwenye alama 57 nafasi ya tatu.

Uwekezaji wa DTB Fc umeonekana kuwalipa maana wamesheheni wachezaji wakubwa na wenye majina ambao wamepita vilabu vikubwa nchini kama Simba, Yanga, Azam, Mbeya city na KMC, lakini pia ina nyota wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali.

Nyota wa DTB Fc wakiwa mazoezini.

DTB inaundwa na nyota kama James Msuva, Juma Abdul, David Mwantika, Yusuph Mlipili na Rajab Zahir. Pia ina nyota wakigeni kama James Kotei, Nicholaus Gyan, Yanick Bazola na Hamis Tambwe.

Mchuano mkali imebaki katika kuwania nafasi nyingine mbili za juu ili kupata nafasi ya kucheza “playoffs” ambapo kuha mchuani mkali kati ya Kitayosce, JKT Tanzania na Mashujaa Fc.

Wachezaji wa DTB Fc wakishangilia baada ya mchezo dhidi ya Pamba kumalizika wa bao moja bila.

Katika vita ya kushuka daraja pia ni Pan Africa wana alama 21 na Mwadui wenye alama 23 sawa na Gwambina na African Lyon  wakiwa wanaburuza mkia lakini wakiwa hawajaachana alama nyingi na African Sports, Ndanda.

Sambaza....