Sambaza....

Falsafa ya Simba ni Kushambulia kwa kulimiliki eneo la kati, na ikitokea Simba wakamilikiwa kati, ujue kutakuwa hakuna ujanja mwingine. Acha tuzitazame mechi hizi ili kuliona hili…

JS SAOURA VS SIMBA.

Katika mechi hii Simba walilala kwa goli 2-0, huku eneo la kiungo wakianza na James Kotei na Jonas Mkude kama viungo wa ulinzi, huku Chama akicheza kushoto na Hassain Dilunga kulia. Meddie Kagere na Bocco kama washambuliaji, huku mabeki wa kati ni Paul Bukaba na Sergie Wawa pembeni ni zana Coulibaly na Mohamed Hussein.

Luis Misuiquone akikaribishwa na kocha mkuu wa Simba sc Sven Van De Broek!

Katika mechi hii Simba walizidiwa umiliki wa mpira na kila kitu.

Umiliki wa mpira :Asilimia 60 kwa 40

Mashuti yaliyopigwa langoni: 19 kwa 7

Mashuti yaliyozuiwa: 6 kwa 1

Mashuti yaliyopigiwa ndani ya Box: 8 kwa 4

Mashuti nje ya box: 11 kwa 3

Jumla ya Pasi zilizopigwa: 472 kwa 306

Usahihi wa pasi: 81% kwa 68%

Kushinda mipira ya 50/50: 62 kwa 42

Kukokota Mpira na kupiga vyenga kwa mafanikio: Kati 27 wamewini mara 16 ikiwa ni sawa na asilimia 59, huku Simba wakifanya hivyo mara 3 bila mafanikio ikiwa ni sawa na asilimia 0%

Katika mechi hii Simba walitawala zaidi upande wa kulia kuanzia kwa Winga Hassain Dilunga, hii iliikuwa ni kipindi cha kwanza kabla ya Aussems kumtoa dakika ya 46 na kumuingiza Haruna Niyonzima lengo ni kuwazuia Saoura kumiliki eneo la kati. Hapo tayari Niyonzima aliungana na Chama eneo la kati, lakini mambo yakazidi kuwa mabaya, ndipo dakika ya 72 akamtoa Chama na kumuingiza Kiberenge Rashid Juma, na baadae kumtoa Mkude na kumuingiza Mzamiru Yassin. Mwisho Simba wanakufa kwa goli 2-0.

Tazama hii, huu ni mkao wa JS Saoura kabla ya kufanya mabadiliko. Hii inatoa maana zifuatazo; kwanza waliingia katika mechi hii kwa lengo la kushambulia, na ndio maana unaona wachezaji wao watano muda mwingi walichezea juu ya Mstari wa kati, pili ni muunganiko mzuri eneo la kati. Ukiitazama timu nzima unaiona jinzi ilivyounganishwa, tazama umbali kati mchezaji mmoja na mwingine… ni mdogo

Wakati huo Simba wao wanawachezaji watatu pekee ambao muda mwingi walichezea juu ya mstari wa kati, ambao ni Dilunga, Bocco na Kagere, Chama, Mkude na Kotei walijitahidi kuwazuia Saoura eneo la kati lakini ilishindikana. Tazama ukaribu wa Zana Coulibaly na Dilunga, hii inamaanisha kuwa, Simba walikuwa wakishambulia sana eneo la kulia kuliko eneo lilingine lile.

Baada ya kipindi cha pili, Simba walijilipua, tazama ramani yao inavyosoma, Wachezaji watano wapo mbele ya mstari wa kati, huku James Kotei akiachwa kumiliki dimba, Mzamiru aliyechukua nafasi ya Mkude akaja kuwa Mshambuliaji, hii ndio maana ya kujilipua hasa baada ya kufungwa goli la pili dakika ya 51 kwa penati ya Mohammed El Amine Ham.

Haya yote namaanisha Fizik ya viungo wa Simba ni mbovu, na kama wataendelea hivi bado kazi ipo. Kuendelea hivi maana yake ni kumilikiwa eneo la kati, eneo ambalo ndilo muhimu sana kwa Simba.

Hapa Zrane, Kocha wa Viungo wa Simba ana kazi ya ziada, kuhakikisha timu inakuwa na msuli, nguvu za miguu na mwili lakini pia Daktari wa Viungo Paul Gomez anatakiwa kuwa mwepesi katika kulishauri benchi la ufundi katika matumizi bora ya wachezaji kulingana na hali zao kiafya, viwango vyao na umri pia.

Ukiachana na endo la kati lakini pia kuna eneo la mabeki. Ukiitazama Simba utabaini kuwa Wabeki wake wa pembeni wana miili midogo, kulia na kushoto, lakini pia ina mabeki wa kati wenye maumbo makubwa, lakini udhaifu wao mKubwa ni kasi, hawana kasi kabisa.

Sven akiwa na timu yake ya ufundi

Kwanini Kasi ni tatizo kwa Simba? Kwa sababu mifumo ya kumiliki  mpira inayotumiwa na Simba inawataka mabeki kuchezea juu ili kulifinya eneo la kuchezea  na kuruhusu kupiga pasi fupi fupi. Kwahiyo Mabeki kazi yao ni kusapoti umiliki wa Mpira.

Huwa ni hatari zaidi timu inapopokonywa Mpira, huku safu ya ulinzi ikiwa juu dhidi ya Washambuliaji wa upinzani wenye kasi kubwa.

Nini kifanyike? Sven anatakiwa kuanza kuchanganya damu hasa katika eneo la Ulinzi sehemu ya Mabeki wa kati kwa maana Kennedy Wilson na Ibrahim Ame kupewa nafasi zaidi ili kujenga uzoefu wa kutosha na kuisaidia timu katika michuano ya Kimataifa.


Soma zaidi


Sambaza....