Baada ya kuwepo na taarifa za hali ya sintofahamu kuhusu mkataba wa Luis Miquissone mchezaji raia wa Msumbiji, mtandao huu uliamua kumuuliza bwana Senzo Mbatha.
Kumbuka Senzo Mbatha ndiye aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba wakati Luis Miquissone na ndiye mtu ambaye alihusika sana kuhakikisha usajili wa mchezaji huyu ukikamilika.
Alipoulizwa na mtandao huu wa kandanda.co.tz, Senzo Mbatha amedai kuwa atajibu kama mtu ambaye alihusika na usajili huo kwa karibu.
“Nitajibu kama mtu ambaye alihusika na usajili wa Luis Miquissone kwa karibu. Sitojibu kwa niaba ya Simba”.
“Luis Miquissone ni mchezaji halali wa Simba na ana mkataba wa miaka mitatu ndani ya Simba kwa hiyo ni mchezaji halali wa klabu ya Simba”- alisema Senzo Mbatha.