Wengi tunafahamu kuwa Luc Eymael siyo kocha tena wa Yanga baada ya Yanga kumfukuza kutokana na kutoa maneno ambayo yalikuwa yana chembechembe za ubaguzi.
Watu wengi walikuwa wanasubiri ni kocha yupi ambaye angekuja kuchukua nafasi aliyoiacha Luc Eymael ambaye ni raia wa nchini Burundi ambaye ni Cedric Kaze.
Luc Eymael aliiongoza Yanga mpaka ikashika nafasi ya pili (2) kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita. Taarifa zinadai kuwa kocha mpya wa Yanga amepatikana.
Kocha mpya wa Yanga inasemekana ni raia wa Burundi ambaye ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burundi ya chini ya umri wa miaka 17.
Kocha huyo aliyezaliwa mwaka 1980 katika jiji la Bujumbura ni moja ya makocha vijana ambao wanafanya vizuri kwenye ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Alianza kazi ya ukocha msimu wa mwaka 2004/2005 akiwa na miaka 25 kwenye klabu ya Prince Louise Rwagasore FC ya nchini Burundi akiwa kama kocha msaidizi.
Msimu wa mwaka 2005/2006 alipewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa Prince Louis Rwagasore FC na aliiwezesha timu yake kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya nchini Burundi nyuma ya Vital’O FC.
Msimu wa mwaka 2006/2007 alienda Atletico FC ya nchini Burundi. Cedric Kaze aliwahi kuwa kocha bora nchini Burundi kwenye msimu wa 2010/2011. Aliwahi kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu nchini Burundi mara tatu ikiwa ndiyo mafanikio yake makubwa.