Sambaza....

Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Parimatch Tanzania imezindua mchezo mpya wa Jackpot ambao utawapa fursa wateja wa kampuni hiyo, kujinyakulia kitita kikubwa cha fedha cha Shillingi Milioni 10 za Kitanzania zitakazokuwa zinatolewa kila wiki.

Jackpot hiyo iliyozinduliwa na Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema kwamba utakuwa mchezo wa kwanza wa Jackpot wenye idadi ndogo ya michezo ya kubashiri nchini na dau dogo zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Maligana amesema kuwa dau la Jackpot hiyo itakuwa ni Shilingi 100 na itakayohusisha mechi 10 za ligi mbalimbali kubwa, ambapo mshindi atapatikana mara baada ya mechi husika kumalizika zilizokuwa zikibashiriwa katika Jackpot hiyo.

“Wateja watatakiwa kubashiri mechi 10 zitakazokuwa zimeorodheshwa kwenye tovuti yetu upande wa Jackpot au wanaweza kuzipata kwa kubonyeza hapa na watafanikiwa kushinda kitita hicho cha Milioni 10 na kubwa zaidi ni kwamba kwa mkeka huo huo mteja anaweza kufanya ‘multi selection’ yaani kuchagua matokeo zaidi ya moja kwa mechi moja. La muhimu pia ni kwamba mechi hizi 10 ni za timu pendwa na za ligi kubwa duniani hivyo uchaguzi utakuwa rahisi zaidi”, amesema Maligana

Aidha, Mkurugenzi huyo Muendeshaji wa Parimatch Bwana Maligana amesisitiza kuwa lengo la kuanzisha Jackpot hiyo ni kutaka kukuza burudani ya soka kwa wateja wa Parimatch ili kusudi wapate fursa ya kushinda kitita kikubwa cha fedha kwa kutoa hela kidogo.

Kwa upande mwingine, Parimatch imekuwa mkombozi mkubwa kwenye soko la michezo ya kubahatisha ndani ya nchini kwa kuweza kutoa michezo na masoko yenye ubora na faida maradufu, malipo kwa haraka baada tu ya mchezo kuisha, huduma ya wateja bora ndani ya masaa 24 siku 7.

Sambaza....