Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Luc Eymael amefungiwa na TFF kutofundisha mpira nchini Tanzania kwa muda wa miaka miwili kutokana na kauli za kibaguzi.
TFF pia imetoa adhabu ya faini ya jumla milioni nane kwa kocha huyo wa zamani wa Yanga. Mpaka sasa hivi Yanga wameshaachana na Luc Eymael baada ya kutoa kauli zenye ubaguzi.