Ligi Kuu Bara imebakiwa na michezo miwili pekee ili kuweza kumalizika, tayari bingwa amepatikana hivyo kubakisha vita katika sehemu mbili pekee kabla ya Ligi kumalizika. Kuna vita ya kuwania ufungaji bora na ile ya kukwepa kushuka daraja.
Baada ya Waziri Junior na Meddie Kagere kufunga katika mchezo wao wa jana tazama hapa chati ya ufungaji bora ilivyonoga haswa kwa wazawa.