Sambaza....

Benard Morrison umejivua nguo hadharani kukataa amri ya mamlaka sahihi inayoendesha shughuli za soka. Ni aibu kwako binafsi, aibu kwa familia yako, aibu kwa timu yako, lakini ni aibu kubwa kwa Taifa unalotoka pia.

Mpira si kitu cha siri kama upo kwenye kiwango bora watu wanaona na kinyume chake kama upo “out of form” kama Jana watu wanaona pia.  Niliwahi kukuelezea ni jinsi gani unajua kucheza mpira kama si kuuchezea mpira lakini una  ujivuni uliopitiliza.

Nafahamu maisha unayoishi na timu yako Yanga yamejaa “udekezwaji” mkubwa sana lakini Jana umekikosea zaidi chombo kinachoendesha mchezo wa mpira wa miguu kwa Mwamuzi wa akiba (4th official) yupo kwa mujibu wa taratibu za mchezo na mchezaji yupo chini ya taratibu za mchezo hadi game inapokwisha.

Benard Morisson.

Timu yako inaweza isikuadhibu kama ilivyo “ada” lakini mamlaka husika itakuadhibu. Nafahamu wewe si mtoto mdogo ni mtu mzima mwenye jukumu ndani ya familia kwa kitendo cha kususa baada ya kutolewa kwa kuchemsha kwenye game unatoa tafsiri gani?

Una binti wa umri wa miaka 8 hope anautambuzi wa mambo ya soka, anaona Baba anafanya nini? Pia unaweka wapi nidhamu ya Wachezaji wote wanaotoka Taifa la Ghana? Unapenda wazungumzwe Waghana hawana nidhamu?nimewahi kuwepo kule nafahamu ustaarabu wa watu wa Ghana na ukarimu wao pia.

Vikosi vya Simba na Yanga vikiingia uwanjani!

Nikukumbushe Derby ya Kariakoo ni moja ya derby kubwa sana Africa inafuatiliwa sana na inatizamwa sana Africa na duniani kote, kwa tendo la utovu wa nidhamu ulioufanya Jana “umejianika” zaidi kama si kujivua nguo mwenyewe, na kuwapa ruksa Wanazuoni waunganishe doti kwenye simulizi za visa vyako maisha ya Career yako na kujua wewe ni mchezaji wa aina gani.

Niseme tena Jana hukucheza vizuri Kocha yeyote asinge sita kukutoa ,hukutimiza wajibu ulicheza 4% ya 10 ulitaka uendelee tuu?.

Sambaza....