KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa anamtazama kwa ukaribu beki wa zamani wa timu hiyo, Abadlah Shaibu ‘Ninja’ ili kuona kama anaweza kufiti kwenye mfumo wake kabla ya kuruhusu asaini dili ndani ya klabu hiyo.
Ninja alikitumikia kikosi cha Yanga msimu wa 2018/19 kabla ya kuondoka na kutua MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Jamhuri ya Czech.Baada ya kujiunga na klabu hiyo, alitolewa kwa mkopo kwenda LA Galaxy ya Marekani kabla ya kurejea kwenye timu yake ya zamani.
Kwa sasa Ninja yupo Tanzania akifanya mazoezi na Yanga. Eymael alisema: “Shaibu kwa sasa sio mchezaji wa Yanga ila amekuja kwa ajili ya kufanya majaribio, ninamtazama ili kuona akikidhi vigezo basi tutamalizana naye.”