Nusu fainali ya kombe la Azam Federation Cup tayari ratiba yake ishatoka , timu ya Sahare All Stars watakutana na Namungo FC. Sahare All Stars ambao wapo ligi daraja la kwanza waliitoa Ndanda FC iliyoko ligi kuu kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Wakati Namungo FC walimtoa Alliance Schools ya Mwanza kwa magoli 2-0. Mchezo mwingine wa nusu fainali ya kombe la shirikisho utakuwa ni watani wa jadi, Kariakoo Derby kati ya Simba na Yanga.
Yanga waliingia kwenye nusu fainali hii baada ya kuwatoa Kagera Sugar kwa ushindi wa magoli 2-1, wakati Simba waliingia nusu fainali hii ya kombe la Azam Federation Cup kwa kuwafunga Azam FC kwa magoli 2-0.
Tarehe 12 watakutana kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo wa nusu fainali , mchezo ambao Simba wanauchukulia kama mchezo wa kisasi baada ya mchezo uliopita kufungwa kwa goli 1-0, kuelekea kwenye mchezo huo Yanga wanaonekana wana ratiba ngumu kuzidi Simba.
Ratiba ya mechi kwa timu zote;
Tarehe 4 Ndanda vs Simba
Tarehe 8 Namungo vs Simba
Tarehe 5 Biashara vs Yanga
Tarehe 9 Kagera vs Yanga
Tarehe 12 Nusu final Fa Simba vs Yanga
Baada ya mechi ya tarehe 9 timu itaondoka Kagera asuhubi ya tarehe 10 na itafika Mwanza mchana na kupanda ndege kuja Dar,Dar timu itafika jioni au usiku kutegemea na booking ya ndege, hapo siku inakuwa imeisha..Kwa maana hiyo timu itafanya mazoezi tarehe11 tuu na tarehe 12 kwenda Taifa kucheza Dar es salaam derby.
*Wakati huo huo Simba watakuwa Namungo tarehe nane,na watafanya mazoezi Dar kuanzia tarehe 09.Kwa maana hiyo Simba itafanya mazoezi ya maandalizi ya derby tarehe 09,10 na 11*