Mshambuliaji wa Totenham Huen Min Son ameelezea hali ilivyokua wakati anatumikia jeshi nchini kwao kwa muda wa wiki tatu baada ya Ligi ya Uingereza kusimama kutokana na virusi vya corona.
Son ambae ni raia wa Korea Kusini alipaswa kuhudhuria kozi ya mafunzo ya kijeshi kama ambavyo sheria za nchi hiyo inavyotaka kila raia wa nchi hiyo kupitia jeshini.
Min Son ameelezea ni kiasi gani aliishi jeshini kwa kipindi chote cha wiki tatu cha mafunzo hayo.
“Sijui jinsi watu [walio na mimi] walihisi, lakini kwangu wiki tatu zimekuwa ndefu, lakini uzoefu mzuri.
Siwezi kusema kila kitu ambacho nimefanya lakini nilifurahia sana. Wale watu walikuwa wazuri, kipindi hicho kilikuwa kigumu, lakini nilijaribu kufurahia.
Siku ya kwanza wakati hatujuani kila mmoja ulikuwa mgumu, lakini baadae tulijuana. Tulitumia siku moja katika chumba kimoja, watu 10 karibu sana, tukifanya kazi pamoja, tukasaidiana ilikuwa ya kupendeza. ”
Nyota huyo wa Tottenham Hotpurs Min Son alitakiwa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi tangu mwaka jana lakini baada ya kuiongoza timu yake ya Taifa Korea Kusini kufanya vizuri katika michuano ya Asia na kuchukua kombe.
Hivyo baada ya Ligi mbalimbali barani Ulaya kusimama ulikua ni wakati sahihi wa Son kulitumikia jeshi kwa wiki tatu baada pia yakupona kutoka majeruhi ya mkono.