Kocha wa klabu ya Yanga Luc Eymael amethibisha kuwa alifanya mawasiliano na wakala wa nyota wa Orlando pirates, Justin Shonga ili kuangalia uwezekano wa kumsajili.
Akizungumza na Jarida la michezo la Kick Off Magazine la Africa Kusini, Eymael alisema kuwa kikwazo kikubwa kilichokwamisha dili la kumsajili nyota huyo wa kimatafa wa Zambia mwenye umri wa Miaka 23 ni kiwango kikubwa cha mshahara anachohitaji kulipwa, Luc alisema Shonga alihitaji kulipwa dola 15000 (R263 362) kwa mwezi ambazo ni zaidi ya milioni 33 lwa pesa za kitanzania.
“Sidhani kama tutaweza kumlipa huo mshahara, Hatuwezi kumudu kumlipa mshahara huo na hata Simba hawezi kulipwa mshahara huo au sehemu yoyote Tanzania lakini ni kama anapenda kwenda Simba, Naona hilo ni tatizo pia.
Inaonekana pia Pirates walihitaji dola za kimarekani 500 000 US dollars [R8.8-million] ili waweze kumtoa kwa mkopo.
Nilijaribu kumpigia Mr [Irvin] Khoza Mara mbili ili tuweze kujadilia hili Jambo lakini sikufanikiwa kumpata,
Nilimpigia Khoza kwasababu wakala wa Shonga aliniambia nimpigie lakini bahati mbaya hakupokea. Nilimtumia ujumbe lakini pia hakunijibu.
“[Bernard] Morrison ni kama amezaliwa upya pale Yanga kwanini isiwezekane kwa Shonga? Lakini sidhani kama atapa hizo dola za kimarekani 15000 anazozihitaji tumlipe, hata Simba hawezi lipwa.
Labda ataenda Simba, Kama ataenda Simba Sina tatizo nae atakuwa mpinzani wetu, Hakuna tatizo” Alisema kocha wa Yanga Luc Eymael