Mlinda mlango wa klabu ya soka ya KMC Jonathan Nahimana ameweka wazi hisia zake na kusema klabu anayoipendelea kuchezea msimu ujao na pia hakusita kuhusu kushindwa kusajiliwa na Yanga kutokana na dau dogo waliloliweka mezani.
Jonathan Nahimana mlinda mlango namba moja wa KMC na timu ya Taifa ya Burundi amekua na kiwango bora msimu huu mbele ya Juma Kaseja na Dennis Richard na kufanya kutawala lango la KMC katika Ligi Kuu Bara.
“Kwa msimu ujao natamani kuichezea Simba ni klabu nzuri yenye kushiriki kimataifa halafu pia ina malipo mazuri, ningepende kuwepo pale ni klabu nzuri kwakweli.” Jonathan Nahimana.
Mlinda mlango huyo ambae alikaa langoni katika mechi zote za Burundi katika michuano ya Afcon mwaka 2019 pia ameweka wazi kwanini alisalia KMC msimu huu na kuacha kusaini klabu za nje na ndani zilizokua zinamuhitaji.
Nahimana “Kuna klabu zingine zilikua zinanihitaji kama Horoya na Nkana Red Devils lakini sikwenda. Kwa hapa nyumbani Azam walinihitaji lakini walikua na kipa Mghana kwaiyo tusingeweza kua “Ma-foreigner” wawili makipa, hivyo wakaniambia mwalimu akiendelea kubaki nisajiliwa msimu ujao.
Yanga pia tulishindwana kwenye maslahi fedha waliyotaka kunipa pia naipata hapa KMC ndiomaana nikaaamua kubaki hapahapa.”
Mlinzi Jonathan Nahimana amebakisha miezi miwili tu kuendelea kuitumikia klabu ya KMC Wana “Kino Boys”.