Sambaza....

Wakati timu Nyingi za soka Afrika Mashariki na kati zikihangaika kutafuta kiungo bora wa kusimamia shoo zote za pale kati uwanjani, Simba inaye fundi Said Hamis Ndemla kwenye Benchi lake ambaye anasimamia shoo mazoezini na benchi.



Ndio, namuongelea yule Ndemla mwingi wa Nidhamu uwanjani, Mwenye mguu wa Dhahabu linapokuja suala la kutwanga mashuti yenye uzito na kupiga pasi ndefu zenye macho, yule yule anaemudu kucheza nafasi zote za kiungo uwanjani kwa ubora wa hali ya juu.

Said Hamis Ndemla.

Ndemla anamiaka zaidi ya sita pale msimbazi lakini hajawahi kuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza, Je tatizo ni nini? Kiwango chake kidogo? Sio chaguo la makocha wote waliokuwepo na waliopo simba? ama haendani na mfumo wa Uchezaji Simba? (Sina jibu).

Ndemla amewahi kwenda nje ya nchi zaidi ya mara mbili kufanya majaribio na timu tofauti, lakini baada ya siku kadhaa unamuona mazoezini msimbazi,na unashindwa kujua nini kimetokea kule, Je hajafuzu vipimo vya Afya?,
Kiwango chake kimekua dhaifu,? au wameshindwana kwenye masuala ya Pesa? (Sielewi).

~~~Tutumie Makala au Uchambuzi kupitia habari@kandanda.co.tz, tutaweka katika sehemu hii ya Kona ya Mshabiki~~~

Ama Simba kuna mzimu Ndemla, kama hachezi kwanini kila mkataba wake ukielekea ukingoni anasainishwa mwingine mpya?, Kwani hakuna Timu zinamtaka? au anafurahia kukaa Simba tu acheze asicheze potelea pwete??, Au hakuna timu nyingine zinaleta ofa kwaajili ya kumnunua?, kwanini Wenzake wanatolewa kwa mkopo timu nyingine lakini yeye ni wa pale pale? (kichwa kinaniuma?).

Umri wake kwa sasa ni miaka 23/24, Ambao kisoka ndio umri mchezaji anapaswa kucheza mechi nyingi ili kujiweka timamu zaidi kimwili, kiakili na hata kupata uzoeufu, Je yeye haoni kama Umri unakimbia na jua linaelekea kuzama?, Au ndio Asharidhika na mafaniko yake kwenye soka tayari?.?

MWISHO, sisi kama mashabiki wa soka safi na wachezaji wenye mvuto kuwatizama uwanjani tunammiss saana Ndemla, Inafika muda tunatamani kwenda mazoezini kuona nini anachokifanya “Ball Dancer” huyu maridadi kabisa..

Mjumbe Hafungwi, Naamini nimefikisha ujumbe kutoka vijiweni mtaani, Mkono wangu wa kushoto unaiweka kalamu chini na kuliacha sikio kuendelea kusikiliza Kibao cha Maalimnash kinachopatikana kwenye mradi wake wa “Diwani ya Maalim”(Album) kiitwacho Dirisha Dogo.

Sambaza....